• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya uwekezaji Uganda yatenga hekari 78.2 kwa ajili ya eneo la biashara

    (GMT+08:00) 2019-09-27 18:25:45

    Mamlaka ya uwekezaji nchini Uganda UIA imetenga hekari 78.2 za ardhi kwa ajili ya ujenzi wa eneo la kibiashara la Oraba katika wilaya ya Koboko nchini humo.Mamlaka hiyo imesema enbeo hilo ni muafaka kabisa kwa wawekezaji wanaolenga nchi za DRC, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati.Akizingumza na waandishi wa habari, waziri wa fedha wa Uganda Bi Evelyn Anite amesema eneo hilo litasaidia pakubwa katika kuimarisha biashara za mipaka. Amesema bidhaa nchi za viwandani vimekuwa vikihitajika katika mipaka ya Sudan Kusini, DRC na Jamhuri ya Afrika ya kati na bidhaa nyingi zinasafirishwa kutoka Kampala Uganda hadi katika nchi hizo.Kwa muda eneo la Koboko limekuwa nyuma kutokana na ukosefu wa viwanda vya kutengeneza bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako