• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NBC yazindua kampeni ya kurahisisha malipo

    (GMT+08:00) 2019-09-27 18:26:25

    Benki ya NBC nchini Tanzania imezindua huduma yake maalumu ya kidijitali ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kurahisisha huduma ya malipo kwa wateja wake wanaofanya miamala ya malipo kwa taasisi mbalimbali ikiwamo malipo ya serikali, umeme na huduma za maji.

    Mkurugenzi wa Idara ya wateja wa kati na wadogo wa Benki ya NBC, Bw Elibariki Masuke alisema huduma inayohusisha usajili wa chini ya muda wa dakika tano tu na inaondoa kabisa matumizi ya karatasi katika usajili ambao hapo awali ulikuwa ukitumia muda mrefu huku pia ukihusisha mahitaji ya nyaraka nyingi.

    Kwa mujibu wa Masuke, huduma hiyo ya Kidijitali itawasaidia wateja wanaolipa ankara za maji, ankara za huduma za televisheni na huduma ya kutuma fedha bila kuhitaji kubeba fedha.

    Alisema kampeni hiyo inafahamika kama 'Kulipa Inalipa' ikimaanisha kwamba mteja wa benki hiyo atanufaika kwa kufanya malipo kupitia huduma hiyo na kwamba mteja anapojisajili kupitia huduma hiyo ataingia moja kwa moja kwenye droo ambayo kila siku itatoa zawadi ya fedha kiasi kisichopungua Sh. 10,000 kwa mshindi.

    Aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo wateja wa benki hiyo wanaepushwa na gharama za kutoa miamala kwenye mashine za kutolea fedha za ATM pamoja na huduma ya mwezi ya kuhudumia akaunti zao isipokuwa watatozwa gharama pale tu watakapotumia huduma za dirishani.

    Mkuu wa Idara ya Huduma za Kidigitali kutoka benki hiyo, Deogratius Mosha, alitoa wito kwa jamii kufungua akaunti na benki hiyo kwakuwa imefanya mabadiliko makubwa kwa kuwekeza kwenye huduma za huduma za kisasa yakilenga kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja wa benki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako