• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kufanya juhudi pamoja na Japan kuhimiza uhusiano kati ya pande mbili kudumisha maendeleo mazuri

    (GMT+08:00) 2019-09-27 19:58:07

    Ubalozi wa China nchini Japan umefanya sherehe ya maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe. Waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe ametuma video ya kupongeza maadhimisho hayo huku akisisitza tena nia ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Japan. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang ameipongeza hatua ya Bw. Abe akisema China inapenda kushirikiana na Japan kuhimiza uhusiano kati ya pande mbili kudumisha maendeleo mazuri.

    Bw. Geng amesema, tunaona kuwa hii imeonesha mwelekeo mzuri wa uhusiano kati ya China na Japan. Mwezi wa Juni mwaka huu, viongozi wa pande mbili wamekutana huko Osaka na wamefikia makubaliano kuhusu kujenga uhusiano kati ya China na Japan unaoendana na zama mpya. Tunapenda kuendelea kufanya juhudi pamoja na Japan kuzidi kufanya mawasiliano mazuri, kudhibiti kiujenzi migongano na kuhimiza uhusiano huo kuendelezwa kwa mwelekeo mzuri juu ya msingi wa kufuata kanuni za nyaraka nne za kisiasa kati ya China na Japani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako