• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la congress la Marekani lamwita Pompeo kufuatia malalamiko ya mfichuzi wa simu tata ya rais Donald Trump

    (GMT+08:00) 2019-09-28 17:18:15

    Wabunge wa Democratic katika baraza la congress la Marekani wamemwita rasmi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kufuatia malalamiko ya mtu aliyefichua siri juu ya simu tata ya rais Donald Trump aliyompigia mwenzake wa Ukraine.

    Hati hii ya wito ni ya kwanza kutolewa na Democratic baada ya Spika wa baraza la Congress Nancy Pelosi kutangaza kuanza kumshtaki rasmi Trump kutokana na mawasiliano yake na Ukraine. Hati ya kumwita waziri huyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kigeni ya baraza la Congress Eliot Engel, akishirikiana na wenyeviti wa kamati nyingine mbili za baraza hilo, inamtaka Bw. Pompeo atoe nyaraka husika katika tarehe iliyopangwa ambayo ni Oktoba 4. Nyaraka hizo zitakuwa sehemu ya mashtaka na kugawanywa kwenye kamati zote.

    Malalamiko ya mfichuzi yalitolewa na afisa wa ujasusi asiyejulikana Agosti 12, yakidai Trump alitumia vibaya madaraka yake kuiomba nchi ya nje kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako