• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHRC yapitisha azimio la haki za maendeleo lililotolewa kwa pamoja na Vuguvugu ya Kutofungamana na China

    (GMT+08:00) 2019-09-28 17:34:51

    Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa UNHRClimepitisha kwa kura nyingi azimio la haki za maendeleo lililotolewa kwa pamoja na Vuguvugu ya Kutofungamana na China.

    Azimio hilo limesisitiza kuwa haki za maendeleo ni haki za watu wote na zisizoweza kunyimwa, ni muhimu katika kutimiza ajenda ya maeneleo endelevu ya mwaka 2030, na kwamba kuondoa umaskini ni kitu muhimu katika kuhimiza na kutimza haki za maendeleo, pia ni sharti la lazima katika kutimiza maendeleo endelevu. Azimio hilo limetoa wito kwa nchi mbalimbali kushikilia sera ya utaratibu wa pande nyingi, kuondoa vikwazo vya maendeleo na kutimiza haki za maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako