• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Kiribati zarudisha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-09-28 17:35:13

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na rais Taneti Mamau wa Kiribati wamesaini taarifa ya pamoja kuhusu kujenga upya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Kiribati kwenye Tume ya Kudumu ya China kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali za nchi hizo mbili zimekubaliana kukuza uhusiano wa kirafiki katika msingi wa kuheshimiana mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutovamiana, kutoingiliana masuala ya ndani, usawa na kunufaishana na kuishi kwa pamoja. Jamhuri ya Kiribati inakiri kuwa duniani kuna China moja, na Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali inayowakilishi China nzima, na Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengeka ya ardhi ya China.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja ni matumaini ya watu na mkondo wa zama hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako