• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liu He kuongoza ujumbe wa China kwenda Marekani kuhudhuria raundi ya 13 ya mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-09-29 19:59:53

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He ataongoza ujumbe kwenda Washington kuhudhuria raundi ya 13 ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kibiashara kati ya China na Marekani.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Shouwen amesema msimamo wa China kwenye mazungumzo hayo ni endelevu na wazi, na kwamba pande hizo mbili zinatakiwa kufanya mazungumzo kwenye kanuni za kuheshimiana, usawa na kunufaishana ili kupata ufumbuzi wa matatizo kati yao, na hii inaendana na maslahi ya nchi hizo na wananchi wao, na pia maslahi ya dunia na binadamu wote.

    Bw. Wang pia amesema China inashikilia msimamo wa kulinda maslahi halali ya kampuni za nje zinazowekeza nchini China, na kutoa huduma bora kwa kampuni hizo kufanya shughuli zao. Amesema katika siku za baadaye China itazidi kufungua mlango wake na kuandaa mazingira ya kibiashara yenye usawa, uwazi na urahisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako