• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara na uwekezaji kati ya China na nchi za "ukanda mmoja, njia moja" vyaimarika

    (GMT+08:00) 2019-09-29 20:01:06

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema biashara na uwekezaji kati ya China na nchi za "Ukanda mmoja, njia moja" vimezidi kuimarika katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

    Bw. Qian amesema mpaka sasa thamani ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda mmoja, njia moja" ni zaidi ya dola za kimarekani bilioni 100, na China imepokea uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 48 kutoka kwenye nchi hizo

    Takwimu zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2013 hadi mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda mmoja, njia moja" ilikuwa zaidi ya dola za kimarekani trilioni 6. China imeanzisha maeneo kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwenye nchi za "Ukanda mmoja, njia moja", na kutoa nafasi laki 3 za ajira kwa wenyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako