• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanamke na mtoto wafariki kwenye ajali ya moto katika kambi ya wakimbizi Ugiriki

    (GMT+08:00) 2019-09-30 09:45:46

    Shirika la habari la Ugiriki AMNA limeripoti kuwa, mwanamke na mtoto walifariki katika ajali ya moto iliyotokea kwenye kambi ya wakimbizi ya Moria kisiwani Lesvos, Ugiriki. Haijafahamika kama marehemu hao ni wa familia moja. Mwili wa mwanamke uliosafirishwa kutoka Kambi ya Moria kwenye Hospitali ya Lesvos umeanza kufanyiwa uchunguzi.

    Chanzo halisi kuhusu ajali hiyo bado haijajulikana. Kwa mujibu wa habari za awali zilizotolewa na mamlaka ya huko, makontena saba yalichomwa moto, na wakimbizi na wahamiaji waliokuwa wanakimbia kutoka kambini hapo walipambana na polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako