• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania bara yaingia Nusu Fanali ya michuano ya Kombe la CECAFA Challenge U20

    (GMT+08:00) 2019-09-30 10:21:58

    Timu ya Tanzania Bara imefanikiwa kuingia Nusu Fanali ya michuano ya Kombe la Matafa ya Afrika Masharki na Kati (CECAFA Challenge U20) baada ya ushindI wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Uganda jana jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Gulu. Mabao ya Tanzania Bara yamefungwa na washambuliaji wake hodari, Andrew Albert Simchimba dakika za 25 na 62 na Kelvin Pius John 'Mbappe' dakika za 89 na 90 na ushei, wakati ya Uganda yamefungwa na Aziz Kayondo dakika ya 46 na 76. Robo Fainali nyingine Sudan imeifunga Sudan Kusini kwa 1-0 Uwanja wa Gulu pia, Kenya imeitoa makamasi Burundi 2-1 na Eritrea ikaishushia kichapo Zanzibar 5-0 Uwanja wa Njeru. Sasa Tanzania Bara itamenyana na Kenya katika Nusu Fainali Jumanne yakiwa ni marudio ya mchezo wa Kundi B ulioisha kwa sare ya 2-2 na Eritrea itamenyana na Sudan, wakati Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako