• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa atangaza kujiweka pembeni kwa miezi miwili ili kupisha uchunguzi dhidi yake

    (GMT+08:00) 2019-09-30 10:22:18

    Baada ya May 30 2017 mbunge wa jimbo la Makindye Magharibi Allan Ssewanyana kupeleka tuhuma zake FIFA kuwa Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda Moses Magogo aliuza kinyume na taratibu tiketi 177 za Kombe la Dunia mwaka 2014 tofauti na ilivyoelekezwa na FIFA, Magogo ametangaza kujiweka pembeni kwa kipindi cha miezi miwili ili kupisha uchunguzi na nafasi yake itakalimiwa na makamu wa Rais wa kwanza wa FUFA. Kwa kawaida FIFA hutoa tiketi za fainali za Kombe la Dunia kila zinapofanyika katika mashirikisho ya soka wanachama, kwa lengo la shirikisho husika kuwauzia raia wa nchini kwake ambao watapenda kwenda kuangalia fainali hizo ila Magogo anatuhumiwa kuuza tiketi hizo nje ya Uganda. Allan Ssewanyana ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo ndio alipelekea tuhuma hizo zilizopelekea Moses Magogo kutangaza kujiweka pembeni kwa kipindi cha miezi miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako