• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawazo ya China ya kujenga ustaarabu wa ikolojia kunufaisha mfumo wa ikolojia duniani

    (GMT+08:00) 2019-09-30 19:20:23

    China inaendelea kuongeza nguvu ya kulinda mfumo wa ikolojia na mazingira, kuanza kushughulikia kwa pande zote mmomonyoko wa udongo na kupanuka kwa jangwa. Tangu mwaka 2000, asilimia 25 ya maeneo mapya yaliyopandwa miti duniani yako China. Idadi ya hifadhi za mazingira nchini China imefikia elfu 2.75. China inaendelea kusukuma mbele juhudi za kushughulikia uchafuzi kwa hewa, maji na udongo ili kupunguza kiwango cha utoaji wa uchafu. Mwaka 2017, fedha zilizotumika kwenye juhudi za kushughulikia uchafuzi wa mazingira nchini China imefikia dola za Marekani bilioni 13.38 ambayo imeongeza kwa mara 300 ikilingana na mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita.

    Mfumo wa maendeleo ya uchumi wa China ulikabiliana na changamoto ya kutafuta maslahi ya muda mfupi bila kujali athari kwa mazingira na maliasili. Lakini kutokana na maendeleo ya jamii, wachina wanaendelea kutilia maanani ulinzi wa mazingira. Rais Xi Jinping amesema maji safi na milima yenye miti ni mali. Maneno hayo yameanzisha msimamo wa kujenga utamaduni wenye mfumo mzuri wa ikolojia. China imeanza kuongeza nguvu ya kulinda mazingira, kuamua kuondoa viwanda vinavyotumia nishati nyingi na kutoa uchafuzi kwa wingi, na kuchagua njia ya maendeleo yenye ubora wa juu ya kuthamani zaidi ikolojia. Hatua za kuhifadhi mazingira na kulinda ikolojia ya China, si kama tu zimenufaisha mazingiraya China, bali pia zimeboresha hali ya hewa na mazingira ya dunia nzima na kutoa mchango katika ikolojia ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako