• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtoto wa Bw. Salim aliyetunukiwa Nishani ya Urafiki na serikali ya China avutiwa na mafanikio ya China katika miongo saba iliyopita

    (GMT+08:00) 2019-09-30 19:27:11

    Bibi Mariam Salim, mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania na mkuu wa shirikisho la urafiki kati ya Tanzania na China Bw. Salim Ahmed Salim, amesema amevutiwa na mafanikio iliyopata China katika miaka 70 iliyopita, ambayo yalipatikana kwa juhudi za wananchi wa China.

    Bibi Mariam Salim ameyasema hayo leo hapa Beijing alipotembelea maonyesho ya mafanikio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Bibi Salim yuko Beijing kwa niaba ya baba yake kupokea Nishani ya Urafiki aliyotunukiwa na serikali ya China. Amesema China imepata maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sayansi, elimu na ujenzi wa taifa. Ameeleza kuwa wazazi wake walishangazwa baada ya kupanda treni ya kasi hapa China, na ni vigumu kwake kuchagua ni ipi inayomvutia zaidi uwanja mpya wa ndege au kilimo cha kisasa.

    "Nishani ya Urafiki" ni tuzo ya ngazi ya juu zaidi ya taifa la China, ambayo inatolewa kwa wageni waliotoa mchango mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa ya China, mawasiliano na ushirikiano kati ya China na nchi za nje pamoja na kulinda amani ya dunia. Kuna wanasiasa na marafiki wanane kutoka nje waliotunukiwa "Nishani ya Urafiki".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako