Mpango huo ulisainiwa na Rais Yoweri Museveni na Benedict Oramah, Rais wa Afrexim. Tawi hilo kampala litakuwa la tano kwa benki hiyo, baada ya Cairo, Abuja, Abidjan na Harare.
Mkataba huo pia unahakikisha Afrexim na maafisa wake wakuu kinga ya diplomasia katika shughuli nchini Uganda.
Tawi la Kampala litafunguliwa kwa biashara mwishoni mwa mwezi Oktoba na litahudumia nchi 11: Kenya, Uganda, Sudan, Eritrea, Djibouti, Ethiopia, Sudani Kusini, Tanzania, Rwanda, Burundi na Comoros.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |