• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wamaliza mjadala wa jumla

    (GMT+08:00) 2019-10-01 08:15:42

    Mjadala wa pamoja wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulimalizika jana baada ya wawakilishi wa nchi zote 192 kuongea kwenye jukwaa la kijani chini ya kauli mbiu ya "kuhimiza juhudi za pande mbalimbali kuondoa umaskini, kuleta elimu bora, kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuleta hali ya ushirikishi.

    Kwenye hotuba ya ufungaji wa mjadala huo, mwenyekiti wa baraza kuu la Umoja wa mataifa Bw. Tijjani Muhammad-Bande, amesema amefurahishwa na mwito kuhimiza dunia ya pande nyingi na kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema alipowasikiliza washiriki amejionea kuwa wanatambua ushirikiano wa pande nyingi ndio njia inayokubalika kusimamia mambo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako