• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Syria na Iraq zaadhimisha ushindi dhidi ya kundi la IS kupitia kufungua mpaka

    (GMT+08:00) 2019-10-01 08:56:19

    Kivuko cha mpaka cha Bukamal-Qaim kati ya Syria na Iraq kimefunguliwa tena, baada ya kufungwa mwaka 2014 wakati kundi la IS lilipokalia eneo hilo la mpakani.

    Mkuu wa idara ya mpaka ya Iraq Bw. Kazm Al-Aqabi na waziri wa mambo ya ndani wa Syria Bw. Mohammad Rahmoun wametangaza kufunguliwa tena kwa kivuko hicho.

    Bw. Rahmoun amesema kivuko hicho ni muhimu kwa shughuli za kibiashara na safari za watu binafsi kati ya Syria na Iraq, na kina umuhimu mkubwa wa kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa nchi zote mbili.

    Kivuko hicho ni moja kati ya vivuko vitatu vikuu vya mpaka kati ya Iraq na Syria, ambacho kinachukuliwa kama moja ya njia kuu za usafirishaji wa mizigo katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako