• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yaiamuru Cardiff City kuilipa klabu ya Nantes dola milioni 6.5 za Kimarekani

    (GMT+08:00) 2019-10-01 10:03:52

    Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiamuru Klabu ya Cardiff City kuilipa Nantes ya Ufaransa dola milioni 6.5 za Kimarekani ili kumaliza mzozo kuhusu malipo ya uhamisho wa Emiliano Sala. Mshambuliaji huyo wa Argentina, Sala alifariki Januari 21 katika ajali ya ndege wakati akisafiri kwenda kujiunga na klabu yake mpya, na awali Cardiff iliamua kutolipa fedha hizo, ambazo ni ada ya jumla ya dola milioni 15 ambazo zilitakiwa kulipwa kwa mafungu, makubaliano yaliyofanyika kabla ya ajali hiyo. Mwaka 2015, Sala alisaini kuichezea Nantes ambako alicheza zaidi ya mechi 100 na kufikia rekodi nzuri ya mabao, akimaliza misimu mitatu mfululizo kwa kuwa mfungaji bora wa klabu. Kiwango hicho kiliifanya Cardiff kumuona na kumsajili Januari, 2019, kwa ada iliyoweka rekodi ya dola 15 milioni. Lakini kabla ya kuanza kuichezea klabu hiyo alifariki katika ajali ya ndege iliyotokea Januari 21, 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako