• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • The Cranes ya Uganda yapata kocha mpya kutoka Ireland Kaskazini

    (GMT+08:00) 2019-10-01 10:04:11

    Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini Uganda (FUFA) Edgar Watson jana alimtangaza Johnny Mckinstry kutoka Ireland Kaskazini kuwa kocha mpya wa The Cranes ya Uganda, na kuziba pengo lililoachwa na Mfaransa Sebastien Desabre. Baada ya kumtangaza Watson alisema anatarajia kuwa kocha mpya itaijenga timu hiyo ili ipate mafanikio zaidi. McKinstry, mwenye miaka 34, aliwahi kuzinoa timu za taifa za Sierra Leone na Rwanda pamoja na klabu ya Kauno Zalgiris ya Lithuania na Saif Sporting ya Bangladesh. Amechukua nafasi ya Desabre, aliyeachia ngazi Julai na kwenda Klabu ya Pyramids FC ya Misri baada ya kuiongoza Uganda kuifikia hatua ya 16 kwenye fainali za Afcon 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako