• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malindi yaungana na Azam, Simba, KMC na KMKM kuaga mapema michuano ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-10-01 10:05:46

    Timu ya Malindi SC imeungana na KMKM, zote za Zanzibar na KMC, Azam FC na Simba SC kuaga mapema michuano ya Afrika kufuatia kuchapwa 3-1 na wenyeji, Al Masry kwenye mchezo wa marudiano Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Borg El-Arab mjini Alexandria, Misri. Matokeo hayo yanamaanisha Malindi inatupwa nje kwa jumla ya mabao ya 7-2, kufuatia kufungwa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Amaan, Zanzibar wiki mbili zilizopita. Katika mchezo huo mabao ya Al Masry yalifungwa na Ahmed Yasser dakika ya nne na 55 na Austin Amutu dakika ya 60, wakati la Malindi lilifungwa na Ibrahim Ali dakika ya 10. KMC ilitolewa na AS Kigali ya Rwanda Raundi ya kwanza, Azam FC ikabanjuliwa na Triangle United ya Zimbabwe Raundi ya Pili. Yanga SC ndio timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika lakini nayo imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zesco Unted Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa. Yanga sasa itamenyana na moja ya timu zilizovuka Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako