• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China asema hakuna nguvu yoyote inayoweza kuizuia China kupiga hatua mbele

    (GMT+08:00) 2019-10-01 11:59:00

    Leo Oktoba Mosi, Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China, na gwaride kubwa la jeshi na maandamano ya umma vimefanyika katika Uwanja wa Tian'anmen katikati ya mji wa Beijing.

    Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti, ambaye pia ni rais wa China na katibu mkuu wa Kamati kuu ya kijeshi ya Chama Xi Jinping, ametoa hotuba muhimu na kukagua gwaride. Amesisitiza kuwa katika miaka 70 iliyopita, kutokana na kuwa na imani ya pamoja na jitihada za pamoja, watu wa China wamepata mafanikio makubwa yanayong'ara duniani. Rais Xi amesisitiza kuwa China imesimama kidete mashariki mwa dunia, na hakuna nguvu yoyote inayoweza kutikisa hadhi ya China, na kuwazuia watu wa China na taifa la China kupiga hatua ya kusonga mbele. Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema kuwa kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China miaka 70 iliyopita, kulibadilisha kikamilifu hatma ya China iliyokuwa maskini, dhaifu na kunyanyaswa, na kufungua njia ya kuelekea ustawi mpya wa taifa la China. Anasema,

    "Katika miaka 70 iliyopita, watu wa makabila mbalimbali ya China wamekuwa na imani ya pamoja na kufanya jitihada kwa pamoja, na kupata mafanikio makubwa yaliyoishangaza dunia. Leo, China ya Ujamaa inasimama kidete mashariki mwa dunia, hakuna nguvu yoyote inayoweza kutikisa hadhi ya China, na wala hakuna nguvu yoyote inayoweza kuwazuia watu wa China na taifa la China kupiga hatua ya kusonga mbele."

    Rais Xi amesisitiza kuwa katika mchakato wa kusonga mbele, China inapaswa kushikilia uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, kushikilia hadhi ya wananchi kuwa mhimili, kutekeleza kikamilifu nadharia, mipango na mikakati ya Chama, kuendelea kukidhi matarajio ya umma juu ya maisha bora, na kuendelea kupata mafanikio mapya ya kihistoria. Anasema:

    "Katika mchakato wa kusonga mbele, tunapaswa kushikilia mkakati wa kutimiza umoja wa taifa kwa njia ya amani na sera ya nchi moja, mifumo miwili, kudumisha ustawi na utulivu wa Hongkong na Macao, kusukuma mbele maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya kando mbili za Mlango Bahari wa Taiwan, kuwaunganisha wachina wote, na kuendelea na jitihada za kutimiza muungano kamili wa taifa. Katika mchakato wa kusonga mbele, tunapaswa kushikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kufuata mkakati wa kufungua mlango kwa msingi wa kunufaishana, na kuendelea kushirikiana na watu wa nchi mbalimbali duniani katika kusukuma mbele ujenzi wa Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja."

    Rais Xi amesisitiza kuwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Kikosi cha Askari Polisi cha Watu wa China (CAPF) wanapaswa kulinda kithabiti mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, na kulinda kithabiti amani ya dunia. Ametoa wito kuwataka wananchi wote wa China kushikamana zaidi, ili kutimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako