• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya nchi mbalimbali vyafuatilia maadhimisho ya Miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China

    (GMT+08:00) 2019-10-01 19:02:43

    Maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yamefanyika leo kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, na kufuatiliwa sana na vyombo vya habari vya nchi mbalimbali.

    Shirika la habari la Uingereza BBC limetangaza moja kwa moja sherehe hiyo, ambapo askari elfu 15 wameshiriki kwenye gwaride na silaha 600 za kisasa zimeoneshwa.

    Gazeti la The Guardian la Uingereza limesema, miaka 70 iliyopita, ndege 17 tu ziliruka kwenye sherehe ya kuanzishwa kwa China mpya. Lakini sasa, kupitia sherehe hiyo, mafanikio makubwa ya maendeleo ya China yameoneshwa, na kwamba mustakabali wa China ni mzuri zaidi.

    Shirika la Habari la Australia pia limetangaza sherehe hiyo na kusema, hotuba ya rais Xi imeonesha kwa wazi imani ya China, hasa aliposema, hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia maendeleo ya China. Kauli hiyo imeonesha viongozi wa China wana uwezo wa kukabliana na hali ngumu ya kipindi cha mabadiliko na imani yao kubwa kwa mustakabali mzuri wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako