• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali yafungua kituo cha kutoa maoni

    (GMT+08:00) 2019-10-01 19:19:12
    Serikali ya Uganda imeanzisha kituo ambapo wananchi watatoa maoni kuhusu uwajibikaji, utenda kazi na huduma.

    Kituo hicho kinalenga kufuatilia utoaji wa huduma za serikali na pia kutumika kama jukwaa la mawasiliano kati yake na wananchi.

    Waziri wa huduma za jumla bibi Mary Karooro Okurut, amesema kituo hicho kitakuwa na njia za kutuma ujumbe kama vile kupiga simu bila malipo kupitia nambari 900, kutuma barua pepe na mitandao ya kijamii.

    Alisema habari zitakazokusanywa zitatumiwa na watunga sera ili kuwezesha serikali kuchukua hatua kulingana na hali halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako