• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Mashariki miongoni mwa maeneo yanayokua kwa haraka kiuchumi

    (GMT+08:00) 2019-10-01 19:19:55
    Nchi za Afrika Mashariki zimeorodheshwa miongoni mwa 20 zenye uwezo wa kukua kwa haraka kiuchumi duniani na kukuza viwango vyao vya biashara licha ya migogoro ya biashara iliyopo eneo hilo na kuongezeka kwa vizuizi visivyo vya ushuru (NTBs).

    Utafiti mpya wa Benki ya Uingereza ya Chartered unaonyesha kwamba Kenya inaongoza kikanda katika suala la kuweka misingi sahihi ya kusaidia ukuaji wa biashara wa siku zijazo kama miundombinu dijitili na sera za urahisi wa kufanya biashara.

    Inafuatwa kwa karibu na Uganda na Tanzania lakini Rwanda na Burundi hazikujumuishwa katika utafiti huo.

    Ulimwenguni kote, Kenya ilishika nafasi ya pili baada ya China na Uganda na Tanzania nayo iko katika nafasi ya 17 na 19 mtawaliwa.

    Tanzania, imepiga hatua kubwa katika kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa nje na na ukuaji wa jumla wa mauzo ya bidhaa za ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako