• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi kuhusisha maeneo mapya matano 

    (GMT+08:00) 2019-10-01 19:20:43
    Kongamano la Kimataifa la Mafuta na Gesi nchini Tanzania kwa mara ya tatu mfululizo litahusisha maeneo mapya matano ikiwamo tuzo tatu kwa kampuni bora zinazofanya vyema kwenye sekta hiyo.

    Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa kongamano hilo, Abdulsamad Abdulrahim alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.

    Mambo mengine mapya ni pamoja na kuwa na uwakilishi wa mjasiriamali kutoka mikoa yote nchini, matumizi ya teknolojia ya mawasiliano wakati wa Kongamano pamoja na utoaji wa zawadi kwa washindi watatu wa uandishi wa Insha.

    Kongamano hilo limeandaliwa Kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Watoa huduma ya Mafuta na Gesi nchini (Atogs), Ewura, PURA, TPDC, pamoja na Kampuni inayoandaa makongamano ya Kimataifa(CWC Group)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako