• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini na Marekani kufanya mazugumzo ya ngazi ya kiutendaji jumamosi wiki hii

    (GMT+08:00) 2019-10-01 20:43:39

    Korea Kaskazini na Marekani zimekubaliana kufanya mawasiliano ya awali tarehe 4 mwezi huu na kufanya mazungumzo ya ngazi ya utendaji siku inayofuata.

    Naibu waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa nchi hiyo Choe Son Hui amesema katika taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Korea Kaskazini kuwa wajumbe wa nchi hiyo wako tayari kuingia kwenye majadiliano ya ngazi ya utendaji.

    Mazungumzo ya kuondoa silaha za nyuklia kati ya Korea Kaskazini na Marekani yamekwama tangu mkutano wa pili kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump uliofanyika Hanoi, Vietnam, kumalizika bila ya kufikiwa makubaliano yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako