• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yamfungia maisha katibu mkuu wa zamani wa CONCACAF

    (GMT+08:00) 2019-10-02 09:06:04

    Naye katibu mkuu wa zamani wa CONCACAF Enrique Sanz amefungiwa maisha na Shirikisho la Soka Duniani FIFA baada ya kukutwa na hatia ya kula rushwa. Kwenye taarifa yake FIFA imesema Sanz mwenye miaka 45 amefungiwa kwa kula rushwa katika mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na FIFA, CONCACAF, Chama cha Soka cha Caribbean (CFU) na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL). Mbali na marufuku hiyo Sanza pia ametozwa faini ya Euro 91,000. Kabla ya kujiunga na CONCACAF, Sanz alifanya kazi na Traffic Sports USA, kampuni ya masoko ya michezo ambayo inahusishwa sana na kashfa za rushwa kwa maofisa wake waandamizi ili kupata haki za matangazo kwenye mashindano makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako