• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya taifa ya waendesha baiskeli wa Rwanda yaelekea Ufaransa kwenye mashindano ya Tour de Vendé

    (GMT+08:00) 2019-10-02 09:06:23

    Waendesha baiskeli wanne wa timu ya taifa ya Rwanda jana walisafiri kwenda Ufaransa kushiriki mbio za baiskeli za Tour de Vendé za mwaka huu zinazotarajiwa kutimua vumbi Oktoba 6. Rwanda itaonekana kwa mara ya kwanza kwenye mbio hizo za kila mwaka, ambazo mwaka huu zinafikisha makala ya 48. Wanne hao ambao wanaongozwa na Samuel Mugisha wanakwenda kuungana na wenzao wawili wanaoishi Ufaransa Moise Mugisha na Jean Claude Uwizeye na kufanya timu ya watu sita. Mashindano hayo makali ya siku moja yatakuwa na umbali wa km 199.5 ambapo nusu yake yatakuwa ni mashindano ya mzunguko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako