• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dwayne Johnson The Rock, atangaza kurejea WWE

    (GMT+08:00) 2019-10-02 09:07:24

    Aliyekuwa nyota wa mchezo wa mieleka Marekani, Dwayne Johnson maarufu The Rock, ametangaza kurejea WWE Ijumaa, Oktoba 4. Bingwa huyo mara nane wa WWE, alitangaza mwezi Agosti mwaka huu alikuwa amestaafu mchezo huo lakini amerejea na atakuwa kwenye kipindi cha WWE Smackdown ambacho kitakuwa kinapeperushwa kwa mara ya kwanza na televisheni ya Fox. Mwanamiereka huyo maarufu, ni muigizaji tajika wa filamu kote ulimwenguni hususan baada ya kuorodheshwa kama muiguzaji anayelipwa zaidi kwa kutia kibindoni mshahara wa Dola milioni 124 kila mwaka. Kupitia Twitter, nyota huyo aliwatangazia wafuasi wake kuwa atarejea uwanjani huku maafisa wakuu wa WWE wakijaribu kuimarisha kipindi hicho kupitia Fox. Mechi yake ya mwisho WWE ilikuwa dhidi ya Erick Rowan ambapo aliibuka mshindi kwa rekodi ya sekunde sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako