• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yemen yatoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kusaidia kuondoa vizuizi vya msaada wa chakula dhidi ya Hodeidah

    (GMT+08:00) 2019-10-02 09:09:58

    Serikali ya Yemen imetoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kusaidia kuondoa vizuizi vya msaada wa chakula dhidi ya mji wa Hodeidah haraka iwezekanavyo.

    Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Bw. Abdul-Raqeeb Fatih amemtaka mratibu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za kibinadamu nchini Yemen Bibi Lise Grande alishinikizie kundi la Houthi moja kwa moja, ili kuondoa vizuizi vya msaada wa chakula dhidi ya eneo la Durayhmi mjini Hodeidah.

    Bw. Fatih akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya utoaji wa msaada wa Yemen, amelaani vikali kundi la Houthi kulizuia Shirika la Chakula la Umoja wa Dunia WFP kuwapatia chakula watu wa Durayhmi.

    Shirika la Habari la Saba pia limetoa taarifa kuihimiza jumuiya ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa kuwaokoa wanaohitaji msaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako