• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia wapongezana katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzisha uhusiano kati ya nchi zao

    (GMT+08:00) 2019-10-02 17:18:24

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wamepongezana kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi zao.

    Kwenye salamu zake za pongezi, rais Xi amesema, katika miongo saba iliyopita, uhusiano kati ya China na Russia umepitia njia ya maendeleo isiyo ya kawaida, na kutokana na juhudi za pamoja za pande mbili, uhusiano huo umekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi kubwa, ujirani mwema na wazo la kusaidiana na kunufaishana. Amesisitiza kuwa anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili na anapenda kushirikiana na rais Putin kuongoza uhusiano huo upate mafanikio mapya katika zama mpya, kushirikiana kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutoa mchango zaidi kwa amani na maendeleo ya dunia.

    Kwa upande wake, Rais Putin amesema baada ya kutafakari mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo, ni wazi kuwa uhusiano huo umefanikiwa kuhimili mitihani ya wakati. Ameeleza imani yake kuwa watafanya juhudi kwa pamoja ili kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zao katika sekta mbalimbali, ili kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili na kuchangia nguvu kwa ajili ya amani na utulivu wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako