• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa juu wa Iran aahidi kupunguza zaidi ahadi zake kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-10-02 19:24:57

    Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema kuwa nchi hiyo itaendelea kupunguza ahadi zake ilizotoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.

    Akizungumza na makamanda wa jeshi la mapinduzi la Iran (IRGC), Khamenei amesema hatua hiyo inapaswa kufanywa kwa uhakika. Amesema Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran linawajibika katika kutekeleza kupunguzwa kwa ahadi hizo kwa uhakika na ukamilifu mpaka nchi hiyo itakapopata matokeo inayotaka.

    Iran ilianza kujitoa kwenye ahadi zake ilizotoa katika Makubaliano ya Pamoja ya Mpango wa Nyuklia wa Iran (JCPOA) baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano hayo mwaka jana, na kuweka vikwazo dhidi ya Iran na kujivuta kwa nchi za Ulaya kutetea maslahi ya Iran chini ya mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako