Hii inalaumiwa kwa kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara na kutokuwa na Brexit, kulingana na Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO).
Biashara ya ulimwengu katika uuzaji inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 1.2 tu mwaka huu, chini ya kiwango cha ukuaji wa asilimia 2.6 iliyotarajiwa Aprili, WTO imesema katika taarifa iliyotolewa.
Biashara ya ulimwengu inatabiriwa kufika asilimia 2.7 mwaka ujao, chini ya asilimia 3 iliyotabiriwa hapo awali.
Mkurugenzi Mkuu wa WTO Roberto Azevêdo amesema mtazamo mbaya wa biashara ndio unavuja moyo.
WTO ambayo inashughuka na sheria za biashara za kimataifa, ilitahadharisha kwamba kushuka kwa kiwango cha chini kunaweza kupunguza nafasi mpya za ajira na kuifanya kuwa ngumu kwa makampuni kutoa bidhaa na huduma kwa masoko kwa ajili ya mauzo ya nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |