• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa wito kuunga mkono ukuaji wa vijana barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-10-03 09:41:39

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun amesema, ili kuhimiza amani, usalama na maendeleo barani Afrika, ni lazima kuunga mkono na kujali ukuaji wa vijana barani humo.

    Katika mjadala wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika, Bw. Zhang amesema Afrika ni bara lenye idadi kubwa ya vijana, na vijana wameshiriki katika ujenzi wa taifa huku wakitoa mchango muhimu katika ustawishaji wa Afrika.

    Amesema kutokana na athari zinazotokana na mapambano ya kisilaha na hali duni ya maendeleo, vijana pia wanakabiliwa na hali ya kuwekwa kando na changamoto kubwa ukiwemo umaskini na ukosefu wa ajira.

    Bw. Zhang amezihimiza pande mbalimbali kuendelea kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo. Ili kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa masuala makubwa, mambo yanahusiana na vijana yanapaswa kuzingatiwa, kusikiliza maoni yao na kuwafanya watumie vizuri uwezo wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako