• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ngorongoro Heroes kukutana na Kenya fainali za kombe la Chalenji U-20

    (GMT+08:00) 2019-10-03 10:38:46

    Timu ya Tanzania Bara Ngorongoro Heroes imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, CECAFA Challenge U20 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Sudan jioni ya jana Uwanja wa Guru nchini Uganda. Sasa Tanzania itakutana na Kenya katika fainali Jumamosi Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), wakati Sudan itamenyana na Eritrea katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu. Katika mchezo wa jana, mabao ya Tanzania Bara iliyo chini ya kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila yamefungwa na Israel Patrick Mwenda dakika ya 36 na Kelvin Pius John dakika ya 45, wakati la Sudan limefungwa na Mohamed Abbas Namir dakika ya 56. Na kwa upande wa Kenya na Eritrea bao pekee walilopata Kenya lilikuwa alilojifunga mchezaji wa Eritrea, Yosief Mebrahtu dakika ya 84. Ikumbukwe Kenya na Tanzania zimetoka kundi moja, B na mechi baina yao ilimalizika kwa sare ya 2-2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako