• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Emmanuel Korir aingia fainali za mita 400 Doha

    (GMT+08:00) 2019-10-03 10:39:03

    Mwanariadha wa Kenya Emmanuel Korir amefanikiwa kuingia kwenye mbio za mita 400 kwa kutumia muda bora katika msimu huu wa dakika 44:37 kwenye nusu fainali zilizofanyika jana Jumatano uwanja wa Khalifa huko Doha. Mkenya huyo anayeishi Marekani amemaliza wa pili katika Heat One nyuma ya Mmarekani Fred Kerley aliyeandikisha muda wa 44.25. Ilikuwa balaa kwa Timu Kenya baada ya Alphas Kishoyian, Mkenya mwingine kumaliza wa sita katika Heat 3 kwenye mbio za nusu fainali zilizomshuhudia Machel Cedenio wa Trinidad na Tobago akishinda kwa kutumia muda wa dakika 44.41. Dakika alizotumia Kishoyian 45.55 hazikutosha kumfanya aingie kwenye fainali. Korir aliwashtua wengi baada ya kushindwa kuingia kwenye fainali za mbio za mita 800 ambapo alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda dhahabu baada ya nyota wa Botswana Nigel Amos kujitoa kwenye mbio hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako