• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya biashara ya UMA yaanza nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2019-10-03 19:30:14

    Biashara ndogo na za kati zitakuwa lengo kuu wakati maonyesho ya 27 ya Chama cha Wazalishaji nchini Uganda (UMA) yaling'oa nanga jana.

    Maonesho hayo,ambayo kwa miaka 27 yameonesha bidhaa za viwanda na uvumbuzi nchini Uganda,yanatarajiwa kuvutia waonyesha bidhaa zaidi ya 500 kutoka nchi 30.

    Haswa maonyesho hayo yatazingatia zaidi uvumbuzi katika biashara ndogo na za kati na pia kusaidia miungano na ushirikiano kutoka makampuni ya kigeni.

    Mwenyekiti wa UMA Bi.Barbara Mulwana aliwaambia waandishi wa habari kuwa maonyesho hayo yatatumika kama jukwaa litakalohakikisha biashara ndogo na za kati zinanufaika pakubwa.

    Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa UMA,Daniel Birungi alisema maonyesho hayo ya siku tisa ambayo yaliaza jana na yatakamilika tarehe 10 Oktoba ni mojawapo ya majukwaa ambayo Uganda inaweza kuonyesha na kupanua uwezo wake wa kiviwanda pamoja na jukwaa la kuzindua bidhaa.

    Miongoni mwa bidhaa zitakazoonyeshwa ni pamoja na pikipiki za kielektroniki,betri za kuchaji,vifaa vya matibabu,transfoma,viti vya plastiki,magodoro,mifumo ya umwagiliaji,vimiminika,malori,vyakula vya kuku na bidhaa nyinginezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako