• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Vyama vya Ushirika na Akiba kukutana Arusha

    (GMT+08:00) 2019-10-03 19:30:42
    Zaidi ya vyama 200 vya ushirika wa akiba na mikopo nchini Tanzania,vitakutana jijini Arusha kuanzia Oktoba 8 hadi 10 ,ambapo pamoja mambo mengine vitatafakari na kushirikishana namna bora ya kufanikisha azma ya utoaji huduma bora na jumuishi za kifedha kwa watanzania.

    Vyama hivyo vinavyoendelea kubadilisha maisha ya watu na kufanikisha ndoto za wananchi na hasa wenye kipato cha chini ndani ya jamii ya watanzania,vinalenga kuwainua kiuchumi kwa kuwahakikishia kipato endelevu kitakachowawezesha kumudu gharama za maisha.

    Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania,Dk Gervas Machimu,jana alisema vya ma hivyo vitakutana katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos) ambayo mwaka huu yanafanyika katika hoteli ya Springs Corridor jijini Arusha.

    Kulingana na Dk Machimu,kupitia siku hiyo,vyama vyote vya ushirika na mikopo Tanzania,vinatafakari namna iliyo bora ya kufikisha huduma za fedha vijijini na kutatua changamoto za mitaji kwa wananchi.

    Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo hufanyika kila alhamisi ya tatu ya mwezi Oktoba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako