• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • USAJILI: Manchester United yaandaa orodha ya wachezaji watatu watakaowasaini dirisha lijalo la usajili

    (GMT+08:00) 2019-10-04 09:43:08

    Manchester United imeandaa orodha ya wachezaji watatu wanaowatarajia kuwasaini dirisha lijalo la usajili ambao ni Ousmane Dembele, Timo Werner na Moussa Dembele. 'The Red Devils' imeandaa orodha hiyo ili kuziba nafasi ya nyota wake waliyemuuza Romelu Lukaku huku Alexis Sanchez wakimtoa kwa mkopo. Meneja wa United, Ole Gunnar sasa amewachagua wachezaji hao watatu akiamini kuwa endapo akipata saini zao basi wanaweza kuipeleka timu hiyo katika 'level nyingine'. Kwa bahati mbaya sana wachezaji ambao kocha, Ole Gunnar amewaorodhesha watahitaji dau nono ili kuweza kukubali kuangusha saini zao ndani ya Old Trafford hii ni kutokana na ubora waliokuwanao. Anthony Martial amekuwa nje tangu mwezi Agosti wakati Marcus Rashford na Mason Greenwood wakiwa bado hawajawa sawa katika 'fitness'. Mashetani hao wekundu wamekuwa wa mwisho miongoni mwa timu ambazo zimeonyesha nia ya kumsaini mchezaji, Martin Odegaard.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako