• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China ahimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza uwekezaji katika kanda ya Maziwa Makuu

    (GMT+08:00) 2019-10-04 18:18:40

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada na uwekezaji katika sekta za mawasiliano, afya na elimu katika nchi zilizo kwenye kanda ya Maziwa Makuu barani Afrika.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kanda ya Maziwa Makuu, balozi Zhang amesema, chanzo kikuu cha mgogoro katika kanda hiyo ni umaskini na maendeleo duni, na njia pekee ya kuondokana na hali hiyo ni kutimiza maendeleo endelevu.

    Bw. Zhang amesema, China inatarajia ofisi ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Kanda ya Maziwa Makuu itahimiza ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za eneo hilo, kuongeza mwingiliano wa miundombinu na kusukuma mbele mchakato wa ujumuishaji ili kutimiza maendeleo endelevu ya uchumi na jamii na kuleta amani katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako