• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Hong Kong yapiga marufuku waandamanaji kuvaa barakoa

    (GMT+08:00) 2019-10-04 18:21:22

    Serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong nchini China imetangaza sheria inayokataza uvaaji wa barakoa, ikiwa ni jitihada mpya za kukabiliana na vurugu zilizodumu kwa muda mrefu.

    Ofisa Mkuu wa mkoa huo Carrie Lam amewaambia wanahabari kuwa, serikali yake imetumia nguvu yake chini ya Mkataba wa Kanuni za Dharura na kupitisha sheria hiyo mpya ili kuweka kizuizi dhidi ya waandamaji wanaovaa barakoa na kufanya vurugu.

    Amesema zuio hilo linatarajiwa kumaliza vurugu na kurejesha utaratibu, na litaanza kutekelezwa saa sita usiku wa leo.

    Vurugu zimetawala mkoa wa Hong Kong kwa zaidi ya miezi mitatu huku waandamanaji wenye msimamo mkali wakiwa na mavazi meusi na kuficha sura zao wakiwasha moto barabarani, kuharibu majengo ya umma ikiwemo vituo vya subway na kuwashambulia polisi, raia, na biashara za watu.

    Msemaji wa ofisi inayoshughulikia mambo ya Hong Kong na Macao ya baraza la serikali la China Bw. Yang Guang leo ametamka kuwa, kuna haja kubwa ya kutoa sheria hiyo, ambayo itasaidia kuzuia vurugu na uhalifu, na kurejesha utaratibu wa jamii mkoani Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako