• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Guniea wabadilishana pongezi kwa miaka 60 tangu nchi hizo kuanzisha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-10-04 18:25:45

    Rais Xi Jinping wa China na rais Alpha Conde wa Guniea wamepeana pongeza kwa miaka 60 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Rais Xi amesema, Guniea ni nchi ya kwanza kuanzisha uhusiano wa kibalozi na China miongoni mwa nchi za magharibi mwa Afrika. Katika miaka 60 iliyopita, ingawa hali ya kimataifa imebadilika, pande hizo mbili zimeendelea kuwa na urafiki wa dhati na kuungana, ambao ni mfano wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo na kuzingatia urafiki wa kijadi kati ya nchi hizo mbili.

    Pia rais Xi amesema anataka kufanya juhudi pamoja na rais Conde kutumia fursa za kujenga Ukanda Mmoja na Njia Moja kwa pamoja na maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na kutoa mchango mkubwa kwa kujenga mustakabali wa pamoja wa China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako