• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uvumbuzi wa teknolojia ni nguvu inayosukuma mbele maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2019-10-06 17:46:12

    Katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, mwanasayansi wa China aliyepewa Tuzo ya Nobel kutokana na utengenezaji wa dawa ya Artemisinin ya kutibu malaria Bibi Tu Youyou alipewa "Nishani ya Juu ya Taifa la China", ambaye mafanikio yake ni mfano mzuri wa maendeleo ya China kwenye sekta ya sayansi katika miaka hiyo 70.

    Mafanikio ya China kwenye sekta ya uvumbuzi wa teknolojia katika miaka hiyo 70 yanatokana na kutiliwa mkazo na serikali ya China. Katika miaka ya karibuni, serikali ya China imekuwa ikitilia maanani uvumbuzi wa teknolojia kwa ajili ya kutimiza matarajio ya wananchi juu ya maisha bora, imeshikilia kuhimiza uvumbuzi kwa mujibu wa mahitaji ya soko, na kuyafanya makampuni yawe nguvu kuu ya uvumbuzi wa teknolojia. Hivi sasa, asilimia zaidi ya 70 ya idadi za gharama ya utafiti, watafiti na haki ya ubunifu nchini China zinatoka kwenye makampuni yake, kama vile Alibaba, Huawei, Tencent, ambayo yamekuwa makampuni bora ya uvumbuzi yenye nguvu ya ushindani duniani, na kuifanya China itangulie duniani kwenye sekta za teknolojia ya kisasa ya akili bandia, 5G, kulipa kwa kutumia njia ya kidigitali, reli za mwendo kasi, magari yanayotumia nishati mpya, teknolojia ya fedha na nyinginezo.

    Katika miaka hiyo 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hasa katika miaka hiyo 40 tangu China ianze sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, China imetoa mchango mkubwa katika kutatua masuala magumu yanayowakabili binadamu duniani kupitia ushirikiano wa teknolojia wa kimataifa chini ya msingi wa kunufaishana. Hivi sasa, watu wote duniani wanakabiliwa na fursa mpya ya mapinduzi ya teknolojia na mabadiliko ya sekta mbalimabali, ukuaji wa uchumi wa dunia uko katika kipindi muhimu sana cha mabadiliko ya nguvu mpya na ya zamani, na uvumbuzi wa China unaendelea kutoa nguvu yake mpya.

    China ikiwa ni nchi kubwa kabisa inayoendelea duniani, kiwango cha jumla cha teknolojia bado kina pengo kikilinganishwa na nchi zilizoendelea. Hata hivyo, China ina uwezo mkubwa kwenye sekta ya uvumbuzi wa teknolojia. China itafuata maendeleo ya teknolojia ya dunia, na kushiriki kwenye mtandao wa uvumbuzi wa teknolojia wa dunia, ili kunufaisha nchi nyingi na watu wengi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako