• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Novak Djokovic achukua kombe la Michuano ya Wazi ya Tenisi ya Japan

  (GMT+08:00) 2019-10-07 10:25:39

  Mcheza tenisi namba moja duniani Novak Djokovic amechukua kombe la michuano ya wazi ya tenisi ya Japan jana Jumapili na kuondoa wasiwasi kuhusu jeraha lake la bega lililomlazimisha kutoka kwenye michauno ya wazi ya Marekani. Nyota huyo kutoka Serbia limtoa kijasho chembamba Muaustralia John Millman kwa seti 6-3, 6-2 na kusherehekea ushindi wake wa 10 kwenye mashindano hayo makubwa. Djokovic, akicheza kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayi, aliwatambia wapinzani wake wiki nzima, bila kupoteza mchezo hata mmoja na hatimaye kujinyakulia kombe katika uwanja wa Ariake Colosseum ambao upo mahsusi kwaajili ya Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020. Djokovic, ambaye ni mshindi wa Grand Slams mara 16, sasa anakwenda kushiriki mashindano ya Shanghai Masters.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako