• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya Mkoa wa Hongkong yalaani vikali vitendo vya kimabavu vinavyofanywa na watu waliofunika nyuso

    (GMT+08:00) 2019-10-07 16:43:39

    Mamlaka ya Mkoa wa Hongkong imelaani vikali vitendo vya kimabavu vilivyofanywa na watu waliofunika nyuso zao ambao waliweka vizuizi kwenye barabara kadhaa za kisiwani Hongkong na Kowloon.

    Watu hao waliharibu zana za umma, vituo vya subway, pamoja na benki na maduka, pia walichoma moto, kutupa mabomu ya petroli, na kuwashambulia wakazi wengine.

    Msemaji wa mamlaka ya mkoa huo amesema, vitendo hivyo vimevuruga vibaya usalama wa jamii, hali ambayo imethibitisha kwamba, mamlaka ya mkoa wa Hongkong ina haja ya kutangaza "Kanuni ya kupiga marufuku kufunika uso".

    Pia amesisitiza kuwa, lengo la kanuni hiyo ni kuzuia vitendo vya kimabavu na kudhibiti vurugu zisizidi kuenea, ili kurejesha amani na utulivu mkoani Hongkong, na kuwataka wakazi wa mkoa wa huo kufuata sheria na kanuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako