• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "China ya Kijani" yaufanya ustaarabu wa kiikolojia wa dunia upendeze zaidi

    (GMT+08:00) 2019-10-07 16:59:49

    Takwimu zilizotolewa na Shirika la anga za juu la Marekani NASA mwezi Februari mwaka huu zimeonyesha kuwa, rangi ya sayari ya dunia imekuwa kijani zaidi kuliko miaka 20 iliyopita, hali iliyosababishwa na kampeni ya kupanda miti na aina mpya ya kilimo yenye ufanisi nchini China na India. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2017, ukubwa wa maeneo ya misitu kote duniani umeongezeka kwa asilimia 5, na China imetoa mchango mkubwa kwa mafanikio hayo tuliyoyapata.

    Juhudi za China katika kulinda maendeleo yasiyosababisha uchafuzi zimesifiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Mafanikio ya China katika kuboresha mazingira ya kiikolojia na kutimiza maendeleo yasiyosababisha uchafuzi yanatokana na mpango wa kimkakati wa serikali ya China pamoja na usimamizi wake mkali juu ya uhifadhi wa mazingira. Katika miaka ya karibuni, China imetunga na kurekebisha sheria tisa za mazingira ya kiikolojia pamoja na kanuni zaidi ya 20 za utawala, ambazo zimekuwa mfumo wa sheria na kanuni unaohusiana na sekta ya mazingira, ikiwa ni pamoja na hewa, maji, ardhi, ikolojia ya kimaumbile, usalama wa nishati ya nyuklia na nyinginezo. Zaidi ya hayo, watu wa China pia wameshiriki kwenye uhifadhi wa mazingira na kuchangia maendeleo yasiyosababisha uchafuzi.

    Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa changamoto ya pamoja inayowakabili binadamu, hivyo ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia unahitaji ushirikiano kati ya nchi mbalimbali duniani. China, ikiwa ni nchi yenye kuwajibika, inashikilia siku zote kupanua ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, imeidhinisha na kutekeleza mikataba zaidi ya 30 ya pande nyingi inayohusiana na mazingira ya kiikolojia. Pia imeshiriki kwenye utatuzi wa mambo ya mazingira ya dunia, na kutangulia kutoa "Mpango wa China juu ya kutekeleza Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030".

    Kwenye mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Septemba, China iliahidi kutekeleza kwa makini "Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa" na wajibu wa "Makubaliano ya Paris", ili kutimiza malengo ya China kwa wakati. Hayo yote yanathibitisha kuwa China itakuwa mshiriki, mchangiaji na kiongozi muhimu kwenye ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako