• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 7 wauawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la Afghanistan mashariki mwa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-10-07 17:00:48

    Wapiganaji 7 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine 7 kujeruhiwa katika mashambulizi makali yaliyofanywa na jeshi la Afghanistan katika mkoa wa Nangarhar, mashariki mwa nchi hiyo.

    Tukio hilo limetokea jana usiku katika eneo la Mirza Ali wilayani Khogyani, ambapo jeshi la Afghanistan lilishambulia kwa risasi maficho ya wapiganaji wa kundi hilo.

    Mapigano makali kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa kundi la Taliban yameendelea katika mikoa 34 ya nchi hiyo tangu mwezi April mwaka huu.

    Kundi la Taliban halijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako