• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CMG na mkoa wa Zhejiang zazidisha ushirikiano wa pande zote

    (GMT+08:00) 2019-10-08 18:37:07

    Hafla ya kusaini makubaliano ya kuzidisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na serikali ya mkoa wa Zhejiang imefanyika leo, ambako pande zote mbili zitahimiza ujenzi wa kituo cha video fupi cha taifa, na kuanza ushirikiano wa miradi mikubwa ikiwa ni pamoja na Michezo ya Asia ya Hangzhou.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema, tangu kuanzishwa kwake, CMG imesukuma mbele ushirikiano wa kimkakati na kanda na sekta mbalimbali. Ushirikiano wa kimkakati na serikali ya mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, ni hatua ya kuboresha mpangilio wa kimkakati na kuhimiza maendeleo yenye ubora, pia ni jaribio la kuonesha thamani ya vyombo vikuu vya habari vya China na kuchangia katika maendeleo ya uchumi ya mikoa mbalimbali, kitendo ambacho kitasaidia mageuzi na maendeleo ya mkoa wa Zhejiang.

    Mkuu wa mkoa wa Zhejiang Bw. Yuan Jiajun amesema serikali ya mkoa huo itachukua fursa hiyo na kujitahidi kuwa kiongozi wa maendeleo ya mafungamano ya vyombo vya habari katika zama mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako