• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CMG yasimamisha tena mpangilio wa matangazo ya Michezo ya NBA mara moja

    (GMT+08:00) 2019-10-08 18:43:08

    Chaneli ya michezo ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG imetoa taarifa tena ya kuamua kusimamisha mpangilio wa matangazo ya Michezo ya NBA mara moja, na kukagua ushirikiano wote unaohusiana na NBA.

    Taarifa hiyo imesema CMG imesikitishwa na kupinga vikali hatua ya Kamishna wa NBA Bw. Adam Silver ambaye yuko nchini Japani ya kuunga mkono kauli isiyofaa iliyotolewa na meneja wa timu ya The Houston Rockets ya Marekani Daryl Morey ya kuunga mkono waandamanaji katika mkoa wa Hong Kong.

    Akieleza msimamo wa Shirika hilo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Geng Shuang amesema haistahili kufanya mawasiliano na ushirikiano na China bila ya kuelewa maoni ya watu wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako