• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga hatua ya Marekani kuziweka kampuni za China kwenye orodha ya kufanya udhibiti juu ya uuzaji wa bidhaa nje

    (GMT+08:00) 2019-10-08 19:28:43

    Wizara ya biashara ya Marekani jana ilitoa taarifa ikitangaza hatua ya kufanyiwa usimamizi na udhibiti kuhusu uuzaji bidhaa nje kwa Idara ya usalama wa umma kwenye mkoa unaojiendesha wa Xinjiang na mashirika yake 18, pamoja na Idara ya usalama wa Kikosi cha uzalishaji na ujenzi cha mkoa wa Xinjiang na makampuni manne ya China.

    Akizungumzia tukio hilo, msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang ameeleza kuwa kitendo hicho kimekwenda kinyume cha kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, kuingilia mambo ya ndani ya China na kudhuru maslahi ya China, na China inapinga kithabiti kitendo hicho.

    Bw. Geng Shuang ameihimiza Marekani ijirekebishe, kufuta uamuzi unaohusika, na kusimamisha kuingilia mambo ya ndani ya China. Amesisitiza kuwa China itaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako