• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Korea Kaskazini na Marekani zitafuata njia ya ufumbuzi wa masuala kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2019-10-08 19:29:13

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang anatumai Korea Kaskazini na Marekani zitadumisha uvumilivu na kusaidiana, na kutafuta ufumbuzi wa masuala yanayoyafuatiliwa na kila upande kwa njia ya mazungumzo.

    Jumamosi iliyopita, Korea Kaskazini na Marekani zimefanya mazungumzo huko Stockholm, Sweden, ambapo Korea Kaskazini imesema mazungumzo hayo hayakuleta matokeo yoyote. Wakati huohuo, Marekani imesema imefanya mazungumzo mazuri na Korea Kaskazini, na kupendekeza kufanya mazungumzo mapya baada ya wiki mbili.

    Akizungumzia hali hii Bw. Geng Shuang amesema, China siku zote inafuatilia mazungumzo kati ya pande hizo mbili. Pia amesisitiza kuwa ni mwelekeo mkuu wa kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea na kudumisha amani kwenye sehemu hiyo, ambayo pia ni matarajio na makubaliano ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako